Musiala akabiliwa na tatizo la kupoteza fahamu

Kiungo wa kati wa Bayern Munich, Jamal Musiala, amegunduliwa kuwa na tatizo la mfumo wa kati wa neva baada ya kuanguka uwanjani kwa mara ya pili ndani ya siku nne.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alianguka dakika sita baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Heidenheim, ambapo Bayern ilishinda mabao 4–2.

Musiala, ambayeni mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, pia alianguka Jumamosi wakati Bayern iliposhinda RB Leipzig 3-1 katika mchezo wa kirafiki.

Kupitia mtandao wa Instagram, Musiala amesema amegundulika kuwa na hali inayoweza kusababisha mtu kupoteza fahamu kwa muda mfupi, kutotambua kinachoendelea au kuonekana kama ameganda kwa sekunde chache.

Musiala ameongeza kusema anafahamu tatizo hilo linaweza kuonekana kuwa la kutisha mwanzoni, lakini kwa sasa ni sehemu ya maisha yake ya kila siku. Na ameanza kupata matibabu.

Kiungo huyo, ambaye tayari amecheza mechi 231 na Bayern, alikosa miezi sita msimu uliopita baada ya kuvunjika kifundo cha mguu kwenye michuano ya Club Cup, lakini alirejea baadaye na kuichezea Ujerumani kwenye Kombe la Dunia la 2026.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii