Uchaguzi wa urais kufanyika wiki hii nchini Zambia

Raia wa Zambia Alhamisi ya wiki hii watapiga kura katika uchaguzi wa rais unaofuatiliwa kwa karibu na ambao utakuwa kipimo cha mafanikio ya kiuchumi ya Rais Hakainde Hichilema anayewania kuchaguliwa kwa muhula mwingine.

Hichilema anakabiliwa na upinzani toka kwa kinara wa upinzani Brian Mundubile, mshirika wa zamani wa rais Edgar Lungu, anayeungwa mkono na muungano wa vyama pinzani, yumo pia Harry Kalaba aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Zambia chini ya utawala wa Lungu.

Wapiga kura milioni 8 na laki 7 wamejiandikisha kushiriki zoezi hilo wengi wao wakiwa wanawake, wataamua kama mageuzi ya kiuchumi ya Hichilema yanastahili muhula mwingine au ni zamu ya upinzani.

Hichilema, kiongozi wa Chama cha United Party for National Development (UPND), alishinda urais mwaka wa 2021 katika jaribio lake la sita, akirithi nchi ambayo haikuwa na uhuru baada ya miaka mingi ya kukopa chini ya Lungu.

Hata hivyo licha ya kufanikiwa kuiondoa nchi hiyo kwenye mdororo wa kiuchumi, Hichilema anashutumiwa kwa kuminya wapinzani wake na kushindwa kutekeleza mabadiliko makubwa aliyoahidi, licha ya kwamba bado anapewa nafasi kushinda kwa muhula mwingine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii