Nchini Uganda, uteuzi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika leo Jumatatu, huku mchakato huo ukikubwa na ukiukaji wa sheria.
Uchaguzi huo, umeanza kwenye mazingira ya machafuko na ukiukaji wa sheria, ambapo kwenye awamu ya kwanza wiki iliyopita, vijiji zaidi ya elfu moja vilishuhudia vurugu.
Hii ina maana kuwa vijiji 1,135 vitalazimika kurudia zoezi hilo Jumanne ya wiki hii.
Sarah Bireete mkurugenzi wa shirika la kiraia linalohusiana na maswala ya utawala na katiba, anasema kuwa uhalali wa zoezi hilo tayari ulitiwa doa kufuatia vurugu hizo.
Mwaka huu uchaguzi huo umeshuhudia vyama vya siasa vikihusika pakubwa,kinyume cha awali ambapo wagombea waliwania nyadhifa hizo bila kuegemea upande wowote wa kisiasa.
Nchini Uganda,viongozi wa mitaa huwa na nafasi muhimu kwenye jamii haswa katika utatuzi wa migogoro.