ufuatiliaji wa tetesi za Ebola umeimarishwa katika jamii na maeneo ya mipakani, ambapo hadi sasa jumla ya tetesi 64 kutoka mikoa 21 zimeripotiwa. Kati ya hizo, wahisiwa 11 walikidhi vigezo vya uchunguzi, walichukuliwa sampuli na baada ya vipimo kuthibitika kutokuwa na maambukizi ya Ebola.
“Mpaka sasa nchi yetu haina mgonjwa wa Ebola na hali ya usalama wa afya nchini iko vizuri. Hata hivyo, Serikali inaendelea kuchukua hatua za mapema na za kina ili kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchini,” amesema Waziri Mchengerwa.
Aidha, amesema Serikali imeimarisha utayari wa wataalamu wa afya na vituo vya kutolea huduma nchini kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa kinga na vifaa tiba muhimu kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo endapo utatokea.Pamoja na hayo amesema seti za kutosha za vifaa maalumu vya kujikinga zinapatikana katika Bohari ya Dawa (MSD) na katika mikoa yote kwa ajili ya matumizi ya dharura, hatua inayolenga kuwalinda wahudumu wa afya waliopo mstari wa mbele.
Katika kuimarisha uwezo wa utambuzi wa ugonjwa huo, Serikali pia imesimika maabara mbili jongezi katika mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kupima sampuli za Ebola karibu na maeneo yanayopakana na nchi zilizoathirika.
Mchengerwa amesema zaidi ya watoa huduma za afya 45,000 wamepatiwa mafunzo ya ana kwa ana na mtandao kuhusu kinga, utambuzi na udhibiti wa Ebola, huku elimu ya afya ikiendelea kutolewa kwa jamii, wasafiri na wananchi wa maeneo ya mipakani.10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii