Mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa kiwango cha njaa kali kinatarajiwa kuongezeka katika maeneo 13 hatarishi duniani katika miezi ijayo.
Mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa kiwango cha njaa kali kinatarajiwa kuongezeka katika maeneo 13 hatarishi duniani katika miezi ijayo.
Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), vita, ukosefu wa fedha na majanga ya hali ya hewa vinawasukuma zaidi mamilioni ya watu katika hali ya njaa kali.
Ripoti ya pamoja ya mashirika hayo inaeleza kuwa hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kati ya mwezi Juni hadi Novemba mwaka 2026, huku takribani watu milioni 266 tayari wakikabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa Sudan, Sudan Kusini, Yemen na Ukanda wa Gaza bado ni maeneo yenye hatari kubwa zaidi ya njaa kali.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime