Maelfu wajitokeza kuuaga mwili wa Khamenei mjini Tehran

Waombolezaji nchini Iran wameendelea kujitokeza kwa wingi mjini Tehran kwa siku ya pili mfululizo katika kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Kiongozi wa juu zaidi nchini humo, Ayatollah Ali Khamenei.

Ibada maalumu ya kumuombea  Khamenei aliyeuwawa katika mashambulizi ya Israel na Marekani mwezi Februari, imefanyika katika Msikikiti wa Grand Mosalla na kuongozwa na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia, Ja'far Sobhani.

Viongozi waandamizi wa serikali wahudhuria

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Iran akiwemo  spika wa bunge  Mohammad Bagher Ghalibaf, wamehudhuria ibada hiyo.

Iran imetangaza Jumapili kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa. Zaidi ya watu milioni 10 wanatazamiwa kushiriki shughuli za kutoa heshima za mwisho. Mwili wa Khamenei utapelekwa Iraq na hatimaye unatarajiwa kuzikwa Alhamisi katika mji wa Mashhad alikozaliwa.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii