Ukraine imetoa tahadhari kwa raia wake wanaoishi katika maeneo yanadhibitiwa na Urusi na kuhamihiza waondoke kuepuka hatari ya mashambulizi ya kutokea angani.
Ukraine imewasihi raia wake kuondoka katika maeneo yaliyokaliwa na kudhibitiwa na Urusi huku mashambulizi yakizidi.
Gavana wa kijeshi wa eneo la kusini mashariki mwa Ukraine la Zaporizhzhya Ivan Fedorov siku ya Alhamisi aliwasihi Waukreni wanaoishi chini ya uvamizi wa Urusi kuondoka huku Kiev ikiongeza mashambulizi ya kutokea angani katika sehemu za nchi zilizokaliwa.
Fedorov alisema kwenye mtandao wa Telegram kwamba vikosi vya Ukraine vinalenga miundombinu ya kijeshi ya Urusi na njia za usambazaji katika maeneo ya Zaporizhzhya na Kherson.
Wakati huo huo, alisema jeshi la Urusi lilikuwa likipeleka vikosi zaidi kulinda vifaa vyake na kuongeza hatari zaidi kwa raia.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime