Watu 20 waangamia kwenye tetemeko la ardhi Ufilipino

Watu 19 wamekufa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kutokea kusini mwa Ufilipino. Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha Ritcher lilisababisha kutolewa onyo la tsunami katika sehemu mbalimbali za eneo hilo.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha Ritcher lilisababisha kutolewa onyo la tsunami katika sehemu mbalimbali za eneo hilo. Tahadhari hiyo iliondolewa saa chache baadaye.

Taasisi ya Volkano na Mitetemeko ya Ardhi ya Ufilipino ilisema kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa kusini-magharibi mwa mji wa Maasim katika jimbo la Sarangani, kwenye kisiwa cha kusini cha Mindanao. Msemaji wa Ofisi ya Ulinzi wa Raia nchini Ufilipino, Junie Castillo, amesema vifo 19 vimethibitishwa hadi sasa, watu 12 hawajulikani walipo na jumla ya 134 wamejeruhiwa. 

Mji wa General Santos, wenye idadi ya watu wapatao 70,000, uliathiriwa zaidi na tetemeko hilo, kulingana na maafisa wa ulinzi wa raia.

Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha majengo kadhaa yakianguka katika eneo la Mindanao nchini Ufilipino. Huduma za umeme na mawasiliano ya simu zilivurugika katika maeneo yaliyoathiriwa, kwa mujibu wa shirika la maafa la Ufilipino. 

Shughuli za masomo shuleni zilifutwa, huku kazi katika ofisi za serikali na za kibinafsi pia zikisimamishwa. Rais wa Ufilipino, Ferdinand Marcos Jr., mara moja aliamuru hatua za msaada na ulinzi na kuwataka watu kufuata maagizo ya mamlaka.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii