Jamaa afariki katika ajali ya barabarani pamoja na mke na watoto 4 baada ya kuongoza sala msikitini

Familia moja imeingia katika maombolezo baada ya kupoteza  ndugu saba kwa wakati mmoja kwenye  ajali mbaya ya barabarani.

Mwanaume, mkewe, na watoto wao walikuwa miongoni mwa waathiriwa waliofariki katika ajali hiyo, na kuwaacha wapendwa wao katika maumivu yasiyoelezeka. Sheikh Mohammed Mamdouh Ali Abdelwahid, kiongozi anayeheshimika na kupendwa katika jamii yake, alifariki papo hapo katika eneo la ajali. 

Kiongozi huyo wa kidini alikuwa ameongoza sala na kutoa khutba ya kidini msikitini saa chache tu kabla ya kukumbana na mauti yake ya kusikitisha. 

“Sheikh alifariki pamoja na mkewe, Jawaria Abu Talib (35), watoto wao wanne, Maryam (14), Talha (10), Aisha (miaka saba), na Hudhaifa mwenye umri wa miaka miwili, pamoja na kaka yake, Ali Mamdouh Ali Abdelwahid (46), ambaye pia alikuwa ndani ya gari hilo.

Familia hiyo ilikuwa ikisafiri katika gari jeusi ambalo lilitoka barabarani na kutumbukia mtoni baada ya ajali hiyo. Kwa kusikitisha, hakuna hata mmoja kati ya waliokuwa ndani ya gari aliyenusurika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii