Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Colombia zimeorodheshwa kuwa miongoni mwa migogoro ya wakimbizi iliyopuuzwa zaidi duniani kulingana na shirika la misaada la Norway, Norwegian Refugee Council (NRC).
Kwa mujibu wa NRC Sudan ambayo tangu mwaka 2023 imekumbwa na vita kati ya majenerali wawili wanaowania madaraka ina zaidi ya watu milioni tisa waliokimbia makazi yao ndani ya nchi wengine milioni nne wamekimbilia nchi jirani huku takriban watu milioni 19.5 wakikabiliwa na njaa.
Mkuu wa NRC, Jan Egeland amesema inashangaza kuona mgogoro mkubwa kama huo ukiendelea bila kupewa kipaumbele cha kutosha duniani, akiongeza kuwa licha ya mahitaji kuongezeka, ufadhili umepungua.
Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako miongo ya vita na mlipuko wa Ebola umeongeza hali ngumu ni asilimia 27.4 tu ya fedha zinazohitajika kwa misaada zimepatikana mwaka 2025 huku zaidi ya watu milioni 21 wakihitaji msaada wa kibinadamu.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime