Serikali ya kijeshi ya Mali imetangaza kitita cha dola milioni 3.5 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa au kuuawa kwa kiongozi wa Al-Qaeda katika eneo la Sahel Iyad Ag Ghaly.
Ghaly kiongozi wa kundi la JNIM anatajwa kuwa mtu anayesakwa zaidi katika eneo hilo kutokana na kuongoza kundi kubwa la wanajihadi linalopambana na tawala za kijeshi nchini humo na katika mataifa jirani.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya usalama zawadi hiyo ni faranga bilioni mbili za CFA huku dola milioni 2.5 zikitolewa kwa taarifa zitakazosaidia kumpata naibu wake Amadou Kouffa.
Pia zawadi nyingine zimetolewa kwa viongozi wa waasi wa Tuareg Mali imekuwa ikikumbwa na machafuko kwa takriban miaka 15 yakihusisha makundi ya wanajihadi wapiganaji wenye uhusiano na Dola la Kiislamu pamoja na magenge ya kihalifu huku nchi ikiendelea kuongozwa na serikali ya kijeshi tangu mapinduzi ya 2020.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime