IAEA yataka kufikia vituo vya nyuklia vya Iran haraka

Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) linadai kuruhusiwa mara moja kufikia zaidi ya vituo kumi vya nyuklia nchini Iran.

Katika miezi ya hivi karibuni Tehran iliruhusu wakaguzi wa IAEA kufika katika kituo kimoja tu cha nyuklia amesema mkuu wa IAEA Rafael Grossi katika ripoti hiyo ambayo bado haijachapishwa rasmi.

Grossi alisema ni "muhimu sana” kwa mdhibiti huyo wa nyuklia wa Umoja wa Mataifa "kufanya shughuli za uhakiki nchini Iran bila kuchelewa,” licha ya kukiri kwamba mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran "yameunda hali isiyo ya kawaida kabisa.

”Iran imepunguza kwa kiasi kikubwa ushirikiano wake na wakaguzi wa IAEA tangu Marekani na Israel zilipoanza mashambulizi dhidi ya nchi hiyo tarehe 28 Februari.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii