Jeshi la Uswisi kupeleka takriban wanajeshi 4,000 mpakani

Jeshi la Uswisi limetangaza kupeleka wanajeshi 4,000 ndani ya mipaka yake kwa lengo la kuimarisha usalama wakati viongozi wa dunia wakitarajiwa kukutana katika mkutano wa kundi la G7 utakaofanyika nchini Ufaransa Juni.

Kwa mujibu wa Jeshi la Uswisi ukubwa wa mkutano huo pamoja na ukaribu wake na mpaka wa Uswisi unahitaji uratibu wa karibu kati ya mamlaka za kiraia na kijeshi ili kuhakikisha usalama unadumishwa katika maeneo yote ya mpakani.

Aidha ripoti zinaonyesha kuwa maandamano yanatarajiwa kufanyika wakati wa mkutano huo  hali inayoongeza umuhimu wa maandalizi ya kiusalama mkutano huo utafanyika kuanzia Juni 15 hadi 17 katika mji wa Evian-les-Bains ulioko kando ya Ziwa Geneva.

Viongozi kutoka mataifa yenye uchumi mkubwa duniani wanatarajiwa kushiriki wakiwemo Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na ujumbe wa ngazi za juu kutoka nchi mbalimbali.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii