Ni baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali dhidi ya Bayern Munich usiku wa kuamkia leo.Sasa watakutana na Arsenal Mei 30 katika mchezo wa fainali ya UEFA.
Mabingwa watetezi wa michuano
ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya UEFA Champions
League, Paris Saint German wametinga fainali ya kombe hilo kwa mara ya pili
mfululizo baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano wa nusu
fainali dhidi ya Bayern Munich usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo PSG walitangulia kupata goli la kuongoza katika dakika ya pili tu kupitia Ousmane Dembele na baadaye katika muda wa nyongeza Bayern Munich wakasawazisha kupitia mshambuliaji wao Harry Kane.
Katika mechi ya kwanza PSG walishinda 5-4 dhidi ya Bayern na hivyo kuwafanya kushinda kwa jumla ya goli 6-5 PSG sasa itacheza fainali ya kombe hilo dhidi ya Arsenal ya England ambayo iliwatoa Atletico Madrid siku ya Jumanne katika mchezo wa fainali utachezwa mjini Budapest, Hungary Mei 30.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime