Vladimir Putin anapunguza idadi ya watu waliokaribu nae, na kusababisha jeshi la Urusi kuwa katika vita vya hatari ambavyo vinatishia kuharibu uchumi wa nchi yake.
Mara chache anaonekana kutengwa zaidi alipoonekana katika matukio mawili ya hivi karibuni, akizungukwa na wasaidizi wake, akiwa ameketi umbali kiasi kutoka washauri wake wa karibu.
Kama Amiri jeshi mkuu, jukumu la mwisho la uvamizi linakua chini yake, lakini daima amekuwa akitegemea watu wake waaminifu, ambao wengi wao pia walianza kazi zao kwenye Idara ya usalama za Urusi. Swali ni nani anaowasikiliza, wakati huu muhimu wa hatima katika urais wake.
Ikiwa kuna anaweza kumsikiliza,basi unaweza kusema ni swahiba wake wa muda mrefu Sergei Shoigu, ambaye ameakisi uamuzi wa Putin wa kuiangamiza Ukraine na kuilinda Urusi dhidi ya tishio la kijeshi la nchi za Magharibi.
Huyu ni mtu ambaye amekuwa akienda katika safari za uwindaji na uvuvi na rais huko Siberia, na katika siku za nyuma ameonekana kama mtu anayeweza kuwa mrithi wake.
Lakini angalia picha yake hii ya kushangaza akiwa mwishoni mwa meza hii, ameketi kwa wasiwasi kando ya mkuu wa majeshi, na unashangaa ni kiasi gani anaweza kusikilizwa na Rais Putin.
Picha hii ilipigwa siku tatu tagu kuanza kwa mashambulio ya kijeshi yanayokutana na upinzani wa Ukraine usiotarajiwa na morali ya chini ya kijeshi.
"Shoigu alitakiwa kuandamana kwenda Kyiv; yeye ni waziri wa ulinzi na alitakiwa kushinda," anasema Vera Mironova, mtaalamu wa migogoro ya silaha.
Alisifiwa kwa kudhibitiwa kwa jeshi la Crimea mwaka 2014. Pia alikuwa msimamizi wa shirika la ujasusi la kijeshi la GRU, akituhumiwa kuhusika kwenye matukio mawili hataeri ya sumu - shambulio la mwaka 2018 huko Salisbury nchini Uingereza na shambulio la karibuni dhidi ya kiongozi wa upinzani Alexei Navalny huko Siberia 2020.
Picha inaonekana kuwa mbaya zaidi ukiitazama kwa karibu. "Inaonekana kama kuna mtu amekufa - inaonekana kama wako msibani," anasema Bi Mironova.
Kama kiongozi mkuu wa wafanyakazi jeshini, ilikuwa kazi yake kuvamia Ukraine na kukamilisha kazi haraka, na kwa kiwango hicho anaonekana hajafikia lengo lililokusudiwa.
Amekuwa na jukumu kubwa katika kampeni za kijeshi za Vladimir Putin tangu alipoongoza jeshi katika Vita vya Chechen vya 1999, na alikuwa mstari wa mbele katika mipango ya kijeshi kwa Ukraine pia, akisimamia mazoezi ya kijeshi nchini Belarus mwezi uliopita.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa kwa sasa kama amewekwa kando kwa sababu ya kuanza kwa kusitasita uvamizi wa Ukraine na ripoti za uwepo wa morali mbaya miongoni mwa wanajeshi.
"Patrushev ni mpenda vita zaidi, akifikiri kwa miaka mingi nchi za Magharibi zinataka kusambaratisha Urusi," anasema Ben Noble, Profesa Mshiriki wa Siasa za Urusi katika Chuo Kikuu cha London.
Yeye ni mmoja wa wafuasi watatu wa Putin ambao wamehudumu pamoja naye tangu miaka ya 1970 huko St Petersburg, wakati mji wa pili wa Urusi ulikuwa bado unajulikana kama Leningrad.
Wachache wana ushawishi mkubwa juu ya rais kama ilivyo kwa Bwana Nikolai Patrushev. Sio tu kwamba alifanya kazi naye katika KGB ya zamani pamoja naye wakati wa enzi za kikomunisti, alirithi nafasi yake ya mkuu wa idara ya usalama, FSB, kutoka 1999 hadi 2008.
Wachunguzi wa mambo wa Kremlin wanasema rais anaamini zaidi taarifa anazopata kutoka Idara ya usalam wa taifa kuliko chanzo kingine chochote, na Alexander Bortnikov anaonekana kuwa sehemu ya watu muhimu wanaomzunguka Putin.
Mtu mwingine muhimu wa muda mrefu kutoka Leningrad KGB, alichukua uongozi wa FSB wakati Nikolai Patrushev alipoondoka.
Wote wawili wanafahamika kuwa karibu na rais, lakini kama Ben Noble anavyosema: "Sio kama tunaweza kusema kwa ujasiri kabisa ni nani anayetoa amri ya kupiga risasi na nani alichukua maamuzi."
Ni mtu muhimu lakini hakuko pale kumpa changamoto kiongozi wa Urusi au kutoa ushauri kwa njia sawa kama ilivyo kwa wengine, anaamini Andrei Soldatov.
Kwa miaka 18 amekuwa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu zaidi wa Urusi, akiwasilisha masuala ya Urusi kwa ulimwengu hata kama hafikiriwi kuwa na nafasi kubwa katika kufanya maamuzi.
Sergei Lavrov, mwenye umri wa miaka 71, bado ni ushahidi zaidi kwamba Vladimir Putin anategemea sana watu wake wa zamani.
Lakini kwa muda mrefu anaonekana kuwekwa kando kuhusu Ukraine na, licha ya sifa yake ya utata na ukali, alitetea mazungumzo zaidi ya kidiplomasia juu ya Ukraine na rais wa Urusi alichagua kumpuuza.
Hakujali wajumbe wengi wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa walitoka nje wakati akijaribu kutetea uvamizi wa Urusi, kwa njia ya video.
Waziri Mkuu Mikhail Mishustin ana kazi kubwa ngumu ya kuokoa uchumi lakini ana ushawishi mdogo kuhusu vita.
Meya wa Moscow Sergei Sobyanin na mkuu wa kampuni kubwa ya mafuta ya serikali ya Rosneft, Igor Sechin, pia wako karibu na rais, kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Yevgeny Minchenko.
Mabilionea ndugu Boris na Arkady Rotenberg, ambao walikuwa marafiki wa utotoni wa rais, kwa muda mrefu wamekuwa marafiki wa karibu pia. Mwaka 2020, jarida la Forbes liliwataja kuwa familia tajiri zaidi nchini Urusi.