Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF limetoa tangazo rasmi kwamba Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya AFCON 2027 yatafanyika kuanzia tarehe 19 mwezi Juni hadi tarehe 17 mwezi Julai mwaka ujao.
Licha ya kutangazwa kwa tarehe hizo, shirikisho hilo halijaweka wazi ni nchi ipi kati ya Uganda, Kenya na Tanzania itakayokuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi na fainali. Tarehe hizo zimeidhinishwa na Baraza la FIFA mjini Vancouver, Canada, baada ya kuondolewa hofu kuwa huenda mataifa yatakayokuwa wenyeji wa michuano hiyo hayatakuwa tayari kwa wakati.
Maandalizi AFCON 2027 yanakwenda vizuri
Rais wa CAF, Patrice Motsepe, amesema maandalizi yanakwenda vizuri na ana imani kuwa mashindano hayo yatafanikiwa. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa michuano ya AFCON kuandaliwa na mataifa matatu kwa pamoja. Itakuwa pia mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika Afrika Mashariki ambapo mara ya mwisho yalifanyika mwaka1976 nchini Ethiopia.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime