Mfumuko wa bei barani Ulaya ulipanda hadi 3% mwezi Aprili

Kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta kutokana na vita kati ya Iran na Marekani kumesababisha kupanda kwa mfumuko wa bei barani Ulaya mwezi Aprili.

Kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta kutokana na vita kati ya Iran na Marekani kumesababisha kupanda kwa mfumuko wa bei barani Ulaya mwezi Aprili, huku ukuaji wa uchumiukiendelea kuwa duni. Hali hiyo imezidisha wasiwasi kwa wateja na watunga sera katika Benki Kuu ya Ulaya.

Mfumuko wa bei katika ukanda unaotumia sarafu ya euro umeongezeka hadi asilimia 3 kutoka 2.6 mwezi Machi, ukichangiwa zaidi na kupanda kwa bei za nishati kwa karibu asilimia 11. Bei ya mafuta ghafi sasa inazidi dola 120 kwa pipa, kutoka takribani dola 73 kabla ya vita kuanza mwishoni mwa Februari.

Vita hivyo vimeutikisa uchumi wa dunia baada ya Iran kufunga Mlango bahari wa Hormuz, njia muhimu inayosafirisha takribani asilimia 20 ya mafuta duniani.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii