Idadi ya watu waliohukumiwa kunyongwa nchini DRC yaongezeka

Idadi ya watu waliohukumiwa kunyongwa nchini DRC imeongezeka tangu kuondolewa kwa marufiku ya hukumu ya aina hiyo mwaka wa 2024 kulingana na ripoti ya shirika moja la kiraia.

Mwaka wa 2024, Congo iliondoa makataa ya sheria ya utekelezwaji wa adhabu hiyo ambayo ilikuwa ikitumika kwa zaidi ya miaka 20, kipindi chote hicho adhabu hiyo iligeuzwa kuwa kifungo cha maisha jela.

Baada ya kuondolewa kwa sheria hiyo, mahakama ziliwahukumu zaidi ya watu 480  kunyongwa.

Kulingana na shirika la Ufaransa la ‘pamoja dhidi ya adhabu ya kifo’ kwa kushirikiana na asasi nyingine za kiraia nchini DRC, tangu kuondolewa kwa makataa hiyo hakuna adhabu ya kifo iliyoripotiwa kutekelezwa.

Ripoti yao imeongeza kuwa, katika nchi ambayo mfumo wake wa mahakama ‘una utata’ na "unaoingiliwa," njia za rufaa zinageuka kuwa ngumu kwa wale ambao hawana wakili, uwezo wa kifedha, au uhusiano na watu wa nje.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii