Bei ya mafuta imeripotiwa kupanda tena kwenye soko la dunia kutokana na athari za moja kwa moja za vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran, ambavyo leo vimeingia siku yake ya 32.
Mapema asubuhi ya Jumanne (Machi 31), pipa moja la mafuta liliuzwa kwa dola 115.17 za Kimarekani kwenye masoko ya Asia, ikiwa ni muda mchache baada ya meli nyengine ya mafuta kushambuliwa kwenye bandari ya Dubai.
Meli hiyo iitwayo Al Salmi ilikuwa imebeba mapipa milioni mbili kutokea Kuwait na Saudi Arabia na mamlaka za Dubai zinasema zinaendelea na juhudi za kuuzima moto uliozuka baada ya kushambuliwa na droni kutokea Iran.
Siku ya Jumatatu (Machi 30), meli nyengine inayomilikiwa na Ugiriki iliripoti kulengwa na makombora mawili ikiwa kwenye pwani ya Ras Tanura nchini Saudi Arabia.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime