ya taa kwa miezi mitatu kuanzia mwezi Machi.
Taarifa
iliyotolewa Jumatatu Februari 28, 2022 na Wizara ya Nishati imesema
kuwa sababu za kuondoa tozo hiyo ni kutokana na kuendelea kupanda kwa
bei za mafuta katika soko la dunia kunakosababishwa na mambo mbalimbali
ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine.
“Pamoja na kwamba uamuzi
huu utaipunguzia Serikali mapato ya kiasi cha Shilingi bilioni 30 kwa
mwezi, Serikali imeona ni muhimu kuendelea kuwalinda wananchi wake dhidi
ya athari za mabadiliko ya bei za mafuta ulimwenguni. Hii inatokana na
ukweli kwamba endapo uamuzi huu usingechukuliwa na Serikali, bei za
mafuta nchini kuanzia mwezi Machi na kuendelea zingekuwa za juu sans
kutokana na sababu zilizoelezwa hapo juu” imesema taarifa hiyo
Taarifa
hiyo imesema kuwa Waziri wa Nishati, January Makamba ameidhinisha na
kusaini marekebisho ya kanuni inayohusika na Tozo hiyo ili kutimiza
uamuzi huu wa Serikali.