EU kutoa msaada wa kibinaadamu wa dola milioni 96 kwa DRC

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa utatoa msaada wa kibinaadamu wa dola milioni 96 ili kuwasaidia watu walioathiriwa na mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Pesa hizo za EU zinalenga kufadhili msaada wa chakula, huduma za afya na kuboresha usafi wa mazingira na makazi pamoja na upatikanaji wa maji mashariki mwa Kongo , lakini pia kuwasaidia wakimbizi wa DRC waliokimbilia katika nchi za Burundi, Rwanda na Tanzania. 

Lahbib amezitaka pande zinazozozana kuyawezesha mashirika ya kibinadamu kulifikia eneo hilo akisisitiza kuwa pesa pekee haziwezi kusitisha mateso ya raia huku akitoa pia wito wa kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinaadamu.

Umoja wa Ulaya umesema kwa sasa zaidi ya watu milioni 21 huko Kongo wanahitaji msaada wa kibinadamu huku wengine takriban milioni 28 wakiwa wameathiriwa kutokana na ukosefu wa chakula kufuatia mgogoro katika eneo hilo lenye utajiri wa rasilimali ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 30.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii