WANANCHI NYAHINGI WAIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE YA MSINGI

Wananchi wa mtaa wa Nyahingi, kata ya Mkolani, wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa Shule ya Msingi Nyahingi ili kuwaondolea watoto wao adha ya kutembea umbali mrefu kufuata shule za mitaa ya jirani.

Wakizungumza na Jembe Habari, wananchi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwasindikiza watoto wao wanapoenda na kurudi shuleni, hususan wakati wa kuwavusha barabara kuu, hatua wanayosema inalenga kuwalinda dhidi ya hatari ya kugongwa na magari.

Aidha wameeleza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwasababishia hofu kubwa juu ya usalama wa watoto wao, huku wakibainisha kuwa kutembea umbali mrefu kila siku huongeza hatari ya ajali, uchovu na kupunguza ufanisi wa wanafunzi darasani.

Akizungumzia changamoto hiyo, Diwani wa Kata ya Mkolani, Juma Mdila, amesema tayari hatua za awali zimeanza kuchukuliwa, akieleza kuwa walikuwa wakisubiri kupatikana kwa bajeti. 

Hata hivyo ameongeza kuwa hivi karibuni wataitisha kikao cha wananchi ili kuwajulisha ratiba ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo.

Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Benson Mwakakongole tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.

Lakini pia tembelea  mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Na @MustaphaKinkulah

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii