Serikali kupitia Baraza la Ushindani (FCT) imeendesha semina kwa wadau wa Mkoa wa Mwanza hatua inayolenga kuimarisha ufanisi wa utekelezaji wa sheria za ushindani katika soko.
Semina hiyo imefanyika leo Februari 5 mwaka huu katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza huku ikihusisha wadau kutoka sekta mbalimbali za biashara.
Akifungua semina hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Balandya Elikana, amesema kuwa semina hiyo ni fursa muhimu kwa wadau wa sekta ya biashara kuelewa majukumu ya Baraza la Ushindani na umuhimu wa kushirikiana katika kutekeleza sheria za ushindani.
Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal – FCT) ni taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, iliyoanzishwa kutatua migogoro ya kiushindani kwa rufaa kutoka kwa taasisi za udhibiti kama Tume ya Ushindani (FCC), EWURA, LATRA, TCAA, na TCRA.
Katibu Tawala huyo ameongeza kuwa semina hiyo itawanufaisha washiriki kwa kuimarisha uelewa wao kuhusu haki na wajibu wao katika masuala ya ushindani, na hivyo kuongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa sheria.
Aidha, wadau wamehamasishwa kutoa maoni na ushauri kuhusu kuboresha mawasiliano kati ya Baraza la Ushindani na sekta mbalimbali, ili kufanikisha malengo ya uwazi na ufanisi katika soko.
Serikali kupitia baraza hilo imeahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu na wadau wote kuhakikisha sheria za ushindani zinatekelezwa ipasavyo, huku mlaji akilindwa na soko likiwa huru na lenye ushindani wa haki.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili mchana ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @Jacob Mlay tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea tovuti yetu ya ,www.jembenijembe.com na mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
Na tunasema Asante kwa time
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime