Mwimbaji maarufu kutoka Nigeria, Davido, ameendelea kukumbana na bahati mbaya katika Tuzo za Grammy baada ya kushindwa kuondoka na tuzo yoyote kwenye toleo la 68 la Grammy Awards 2026, licha ya kutajwa kwenye vipengele vitatu (3).
Kupitia chapisho lake la Instagram, imeonekana wazi kuwa staa huyo hakuwa na hamu kabisa ya kuhudhuria hafla hiyo, akihisi safari hii pia mambo yangeenda kombo. Hata hivyo, msukumo kutoka kwa mke wake, Chioma, ulimfanya abadili mawazo na kuamua kujitokeza.
umeendelea kuwa kitendawili kigumu kwake.
Hata hivyo, mashabiki wake wengi wanasema:
“Nominations pekee ni ushindi tayari. Afrobeat inaendelea kufika mbali kwa sababu ya Davido.”
Na ukweli ni kwamba, licha ya kukosa tuzo, mchango wake kwenye muziki wa Afrobeat duniani haupingiki. Amezidi kufungua milango kwa wasanii wa Afrika kwenye soko la kimataifa.
Wengine wanaamini huu ni muda tu, siku yake ya kunyanyua Grammy itafika.