Davido akosolewa kwa kulaani utekaji nyara wa wanafunzi

siasa za Nigeria zinaingilia tasnia ya burudani na ulimwengu wa muziki. Miezi saba kabla ya uchaguzi mkuu ujao, chama tawala cha All Progressives Congress (APC) kinashutumiwa kwa kuwashinikiza wapinzani wake wa kisiasa kwa njia yoyote ile.

Siku ya Jumanne, Juni 16, 2026, mahakama ilibatilisha uamuzi wa kutoshiriki katika uchaguzi wa dakika za mwisho kwa vyama vitano vya upinzani, saa 24 baada ya uamuzi tata ambao ungeviondoa kwenye uchaguzi ujao. Siku ya Jumatano, Juni 17, 2026, mwanamuziki maarufu Davido alijikuta akikosolewa na mwanamuziki mwingine, mfuasi wa Rais Tinubu. Mwanamuziki huyu alimshutumu nyota huyo kwa kuchafua taswira ya Nigeria wakati wa onyesho nchini Marekani wiki iliyopita.

Mnamo Juni 10, kama sehemu ya tamasha la kimataifa lililoandaliwa na Shirikisho la Soka la Dunia, FIFA, kuzindua sherehe za Kombe la Dunia la Soka, mwanamuziki nguli kutoka Nigeria, Davido, alitumbuiza huko Los Angeles. Kwa onyesho lake, alivalia koti jeusi la ngozi, lililopambwa na beji takriban arobaini za kijani, kila moja ikiwa na jina la mwanafunzi au mwalimu aliyetekwa nyara wakati wa shambulio dhidi ya shule tatu katika jimbo la Oyo mwezi Mei.

Nyuma ya koti hii, maneno matatu yaliandikwa: "Bring them home" (kwa Kiswahili "Warudisheni nyumbani"). Ujumbe ambao Davido aliurudia kwenye kipaza sauti.

Lakini mpango huu ulikosolewa vikali siku ya Jumatano, Juni 17 na mwanamuziki mwingine, Dauda Rarara, aliyetambuliwa kama mfuasi wa muda mrefu wa chama cha Progressive Congress, APC, chama cha wengi.

Anashtumiwa kwa "kuingiza siasa" katika tamasha lake

Katika video kwa lugha ya Kihausa, anamuelezea Davido kama "mshenzi" na hata "mchochezi wa ugaidi", na anamshutumu kwa kuchafua taswira ya Nigeria kwenye anga za kimataifa. Kulingana naye, nyota huyo alitaka "kutumia siasa" ili ajionyeshe kwa sababu mjomba wake, Ademola Adeleke, ni gavana, mwanachama wa upinzani.

Davido alijibu kwenye mtandao wa kijamii X, akisema kwamba "mzalendo wa kweli wa Nigeria (...) hawezi kukaa kimya kwa matatizo ya usalama yanayoikumba nchi na hapaswi kuwazuia wengine kuwa na wasiwasi kutokana na hali hiyo."

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii