AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA KAKA YAKE,

Mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya msingi Mwenge manispaa ya Morogoro Faidhati Ibrahim Gadafi (13 )ameuawa kwa kukatwa na mapanga na kaka yake anayetambulika kwa jina la Shomari Malima mtoto wa mama yake mkubwa akiwa nyumbani kwao mtaa wa Tambukareli kata ya Kingolwila Manispa ya Morogoro huku sababu ikitajwa ni ugomvi wa kifamilia wakigombania Mali za urithi pamoja na Ushirikina.

Aidha chanzo cha tukio hilo ni kwamba kuna mgogoro mkubwa sana wa kuwania mali za marehemu babu na marehemu bibi, lakini pia polisi wamebaini kuwa kuna mgogogro mwingine wa imani za kishirikina zilizopelekea baadhi ya watoto kufariki katika familia hiyo na kuhusishwa mama mzazi wa binti huyo aliefariki kuwa ameshiriki katika mauaji hayo.

Lakini pia sababu nyingine iliyopelekea mauaji hayo ni kwamba kijana aliyefanya mauaji hayo ana matatizo ya kiafya ambapo alipata tokea anazaliwa na matatizo hayo ni ukosefu wa nguvu za kiume

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii