Vyombo vya habari vimeripoti tukio la kuuwawa kwa mwandishi wa habari kulikotokana na shambulizi la Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza,
Wakati huohuo shirika la habari la Palestina WAFA likitoa taarifa ya kujeruhiwa kwa mwandishi mwingine kwa shambulizi la droni huko katika mji wa kusini wa Khan Younis. Msemaji wa jeshi la Israel amesema vikosi vya jeshi vinafanyia uchunguzi taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa WAFA, mwandishi aliyeuawa alitajwa kwa jina Mahmoud Wadi. Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilisema kwamba alikuwa akitumia kamera ya droni katika kazi yake kwa vyombo mbalimbali vya habari.
Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi wa Habari (CPJ) inasema kwamba zaidi ya waandishi wa habari 200 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa mzozo huo zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina Hamas yamekuwepo tangu Oktoba 10, lakini matukio ya vifo yanaendelea kutokea.
Israel imekuwa ikiwalaumu mara kwa mara waandishi wa habari katika Ukanda wa Gaza kwa kufanya kazi kwa niaba ya Hamas.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime