BARAZA LAMCHAGUA SARA NG'HWANI KUWA MEYA

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza limempitisha Diwani wa kata ya Buswelu Bi  Sara Poul Ng'hwani kuwa Meya wa Manispaa hiyo baada ya kupata kura 27 na hakuna kura iliyoharibika katika kura zilipigwa leo.

 Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo , Bi Sara Ng'hwani amesema kuwa atashirikiana vyema na madiwani wenzake ili kutatua changamoto za wananchi kupitia utekelezaji wa sera walizoziahidi  katika kampeni za uchaguzi uliofanyika mwaka huu.

Pia baraza hilo limemchagua diwani wa viti maalamu, Kuluthumu Salumu Abdalah kwa kupata  kura 24 kati ya kura 27, kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya halmashauri ya wilaya ya Ilemela ameahidi kushirikiana na madiwani wenzake na viongozi wengine katika kutumikia wananchi wake na kulinda amani ya nchi

Aidha, kikao hicho kiliambatana na zoezi la kuapisha  madiwani na hii ni hatua ya kuwezesha viongozi hao kuanza kutekeleza majukumu yao kwaajili ya kuwatumikia wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii