Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anatazamiwa kushinda muhula wa nne madarakani, wakati matokeo ya awali yakiashiria ushindi wa kishindo katika uchaguzi ambao wapinzani wake wakuu walipigwa marufuku kugombea.
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anatazamiwa kushinda muhula wa nne madarakani, wakati matokeo ya awali yakiashiria ushindi wa kishindo katika uchaguziambao wapinzani wake wakuu walipigwa marufuku kugombea.
Ouattara aliye na umri wa miaka 83, ameliongoza taifa hilo mzalishaji mkuu wa Cocoa duniani tangu mwaka 2011, wakati nchi hiyo ilipoanza kujiimarisha kama taifa lenye nguvu kiuchumi Afrika Magharibi.
Matokeo rasmi kutoka maeneo ya kaskazini ambako ni ngome kubwa ya Ouattara yalionyesha ushindi wa hadi asilimia 90 huku idadi ya wapiga kura waliojitokeza ikikaribia asilimia 100.
Kigogo huyo pia alikuwa akiongoza katika maeneo ambayo kijadi ni ya upinzani upande wa kusini na baadhi ya maeneo ya jiji la kiuchumi la Abidjan ambako vituo vya kupiga kura vilikuwa karibu vitupu siku ya jumamosi.