Serikali mpya ya Peru imetangaza siku ya Alhamisi nia yake ya kutangaza hali ya hatari katika mji mkuu, Lima, kufuatia wimbi la ghasia za uhalifu zilizopangwa ambazo zimesababisha maandamano makubwa yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja na karibu 100 kujeruhiwa.
"Tutatangaza uamuzi wa kutangaza hali ya hatari, angalau katika mji wa Lima," kiongozi wa serikali ya mpito Ernesto Álvarez amewaambia waandishi wa habari baada ya mkutano wa baraza la mawaziri.
Hatua hii itaathiri watu milioni 10 wanaoishi katika mji mkuu na bandari ya karibu ya Callao.
Siku ya Jumatano, maelfu ya waandamanaji waliandamana kote nchini kupinga kukithiri kwa ukosefu wa usalama. Huko Lima, makabiliano kati ya polisi na waandamanaji, ambayo ni ghasia zaidi tangu kuanza kwa maandamano ya kila siku mwezi mmoja uliopita, yalisababisha kifo cha mtu mmoja, aliyeuawa na polisi, na angalau 113 kujeruhiwa, wengi wao wakiwa maafisa wa polisi, kulingana na takwimu rasmi.
Chini ya hali ya hatari, serikali ina uwezo wa kutuma jeshi kushika doria mitaani na kuzuia baadhi ya haki, kama vile uhuru wa kukusanyika.
"Marufuku ya kutotoka nje sio huenda ikatangazwa (...) ikizingatiwa kuwa uhalifu" mara nyingi unatekelezwa na "usiku," ameongeza Ernesto Álvarez.
Mkuu wa ofisi ya rais ameongeza kuwa serikali itatangaza katika siku zijazo safu ya hatua ambazo zitaambatana na hali ya hatari ya siku zijazo.