Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Syria, Noureddine al-Baba, amesema uchaguzi wa bunge nchini humo umekamilika katika vituo vyote vya kupigia kura bila tukio lolote la kuhatarisha usalama.
Noureddine al-Baba amesema wizara hiyo ilihakikisha usalama katika vituo vyote 50 vya kupigia kura vilivyotawanyika kote nchini, na kulinda zaidi ya maafisa 7,000 wa kamati ya uchaguzi.Al-Baba amesisitiza kuwa huo ni uchaguzi wa kwanza nchini Syria kufanyika bila kuingiliwa na vyombo vya ujasusi au maafisa wa serikali katika uteuzi wa wagombea, na kwamba mchakato huo umefanyika kwa uhuru.Syria imefanya uchaguzi wa bunge Jumapili hii kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Bashar al-Assad, hatua muhimu katika kipindi cha mpito cha taifa hilo baada ya takriban miaka 14 ya vita.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii