Aliyekuwa mmiliki wa Home Grand Hotels, TCCIA Region Treasurer, na mfadhili wa CCM Wazazi, Kevin Williams Mbogo, amefariki dunia kwa ajali ya gari usiku leo Oktoba 4 mwaka huu katika eneo la Sayansi, jijini Dar es Salaam.
Marehemu aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Katavi kati ya mwaka 2012 hadi 2017, akiwa na mchango mkubwa katika siasa za vijana na jamii kwa ujumla.
“Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi.”