Jeshi la Israel limesema Jumatano litaifunga njia ya mwisho iliyosalia kwa ajili ya wakaazi wa kusini mwa Gaza kuelekea kaskazini, huku likiendeleza mashambulizi yake Gaza City.
Msemaji wa Jeshi la Israel kwa lugha ya Kiarabu, Avichay Adraee amesema Barabara la Al-Rashid itafungwa kuanzia majira saa sita mchana saa za Mashariki ya Kati.
Adraee ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba watu wanaoelekea kusini ambao hawakuweza kuhama Gaza City wataruhusiwa kupita.
Amesema jeshi la Israel linaruhusu watu kupita kuelekea kusini bila kukaguliwa.
Ujerumani yaidhinisha mauzo ya silaha kwa Israel
Wakati huo huo, serikali ya Ujerumani imeidhinisha mauzo ya silaha kwa Israel yenye thamani ya euro milioni 2.46.
Kwa mujibu wa Wizara ya Masuala ya Kiuchumi, uidhinishaji huo umefanyika tangu Ujerumani ilipositisha kwa sehemu mauzo ya silaha kwa Israel.
Kulinga na wizara hiyo, mauzo hayo yanahusisha bidhaa nyingine za kijeshi, na hazijumuishi silaha za kivita.