Mwalimu akamatwa kwa madai ya kumpiga mtoto viboko hadi kufa

Mwalimu wa shule amekamatwa nchini Nigeria kwa madai ya kumpiga mwanafunzi wa miezi 19 hadi kufa, polisi wanasema.

Mwalimu huyo katika shule ya msingi ya Asaba, jimbo la Delta, alidaiwa kuacha alama nyingi kwenye mwili wa mtoto huyo baada ya kumchapa viboko Jumatatu iliyopita.

Mshukiwa huyo anayedhaniwa kuwa mtoto wa mmiliki wa shule hiyo ya kibinafsi, anadaiwa kuanza kumpiga mwanafunzi huyo baada ya kumshika akicheza na maji.

Hajaripotiwa kuzungumzia tukio hilo.

Mwanafunzi huyo alisemekana kuugua baada ya tukio hilo na alipelekwa katika Kituo cha Afya cha Shirikisho (FMC) huko Asaba ambapo hatimaye alifariki.

Msemaji wa polisi DSP Dafe Bright alisema kwamba mshukiwa atashtakiwa kwa mauaji bila kukusudia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii