Mwabukusi atoa Tamko kuelekea Uchaguzi mkuu

Rais wa Tanganyika Law Society (TLS), Boniface Mwabukusi, ametoa mtazamo kuhusu uhusiano kati ya haki, amani, na mchakato wa uchaguzi nchini. Mwabukusi alisisitiza kwamba amani haiwezi kuwepo bila haki, akilinganisha amani bila haki na “illusion” kitu kisicho na msingi. 

“Amani ni macho haki ni nuru ukiwa na macho hakuna nuru huwezi kuona. kwa hiyo hakuna amani unayoweza kuizungumzia bila kuwa na haki kwa lazima uanze na haki kufikiri” alisema.

Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao, Mwabukusi alisema TLS imefanya kazi kubwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya amani, haki, na utulivu. Alieleza kwamba TLS ilipokea na kuchunguza malalamiko mbalimbali kuhusu mchakato wa uchaguzi, ikiwemo malalamiko kuhusu marekebisho ya sheria na ushiriki wa wananchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii