SHIRIKA la Bima Zanzibar (ZIC)
Februari 10 limekutana na kuzungumza na Mawakala na Madalali wa shirika
hilo katika kikao kilichofanyika Hoteli ya Cate Jijini Dar es Salaam.
Aidha
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) Araf Haji
amesema Mwaka huu wamejikita zaidi Katika kuboresha Huduma kwa wateja
na kurahisisha upatikanaji wa Bima hasa kwa kujikita katika kutoa huduma
kwa njia ya Mtandao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Bima Zanzibar (ZIC) Arafat Haji akikabidhi Cheti Kwa Moja ya wakala wa
Bima Kwa kutambua Mchango wake katika utoaji wa Huduma zao za Bima
mara baada ya kumaliza kikao kilichowakutanisha Mawakala pamoja na
uongozi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC ) jijini Dar es salaam.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Uongozi wa
Shirika hilo ukiongozwa na Mkurugenzi huyo akiambatana na Meneja wa
Kanda ya Pwani Majda Issa Ahmed na Ndugu, Mohammed Ameir Mkurugenzi
Biashara (ZIC).
Aidha Haji amefafanua zaidi kuwa kikao hicho
kimeazimia kuwa na Mategemeo ya kuboresha Mahusiano Mazuri kati ya
Shirika hilo pamoja na Mawakala hao na kuongeza ukuaji wa Biashara.
"Tunategemea
Mahusiano haya ambayo yamejengeka yataweza kusaidia kuboreshwa Kwa
Huduma pamoja na changamoto zilizowasilishwa zitaweza kutatuliwa Kwa
haraka na nawasihi muendelee kuwa mabalozi wazuri wa ZIC."
Kwa
upande wake Meneja wa Shirika hilo Sabri Ali amesema kikao hiko kimekuwa
chenye Manufaa kutokana na Madalali hao kuwasilisha changamoto zao
hivyo kama Shirika limeweza kufikishiwa changamoto hizo na kuahidi
kuzitatua Ili kuleta ufanisi wa huduma Kwa wateja.
Sabri amesema
Shirika lipo mbioni kuongeza huduma nyingine na Bima ya usafiri hasa
usafiri kwa wasafiri waendao nje ya Tanzana pamoja na kuleta huduma ya
bima ya Afya Kwa wateja wao ili kuwahakikishia wanapata huduma zilizo
bora zaidi .