humu duniani hapakosi vituko. Pasta mmoja wa kuhubiri mitaani amewashtua wengi na mahubiri yake tatanishi kuwa waume wanao wapachika mimba wake zao wanatenda dhambi.
Vile vile pasta huyo amewaonya watu wanaokunywa dawa na wanaotafuna chingamu kuwa ni dhambi.
Katika video, pasta huyo anaonyeshwa akiubiri katika kituo cha mabasi katika moja ya majimbo ya Nigeria.
Wakati alikosolewa na baadhi ya abiria kuhusu mahubiri yake, mhubiri huyo anasikika akisema kuwa ndoa si dhambi lakini mume kumpachika mke wake mimba ndio dhambi.
Aliendelea kufafanua kauli yake akisema: "Si wanawake wote wanaofanya mapenzi hupata mimba na hivyo wanaume wanapaswa kuomba msamaha baada ya kuwapa mimba wake zao kwa sababu kupata watoto si lazima”.
Pasta huyo pia aliongeza kuwa kuvaa longi, kutumia mikorogo, kuvaa saa za mikononi na pete zote ni dhambi.
Isitoshe, pia anasikika akisema kuwa mwanamume ambaye anamkumbatia mwanamke ambaye hajamwoa ni dhambi na lazima atoe mahari kabla kufanya hivyo.
Alimuomba kila mtu kutubu na kurekebisha njia zao kwani giza linakuja.
Kwingineko, video ya pasta mmoja akiwapa kondoo wake kidole chake walambe kama komunyo imezua ghadhabu kwenye mitandao ya kijamii.
Pasta huyo alikuwa akiwalambisha waumini kidole chake baada ya kula chakula aina ya eba na supu kwenye madhabau.
Mchungaji huyo mwenye utata alirudia utaratibu huo kwa washarika wote walipokuwa wakienda madhabahuni mmoja baada ya mwingine kupokea 'meza ya Bwana.