mafuriko yaua watu 119 Taxes Marekani

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko makubwa huko Texas, Marekani imeongezeka hadi kufikia watu 119

Hata hivyo wasiwasi umezidi kuongezeka kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu kwa kuwa hadi sasa zaidi ya watu 160 bado hawajulikani walipo.

Maafisa zaidi ya 2,000 wa vikosi vya uokoaji, polisi na wataalam wengine wanaendelea kuwatafuta manusura kufuatia mafuriko ya Julai 4 huku Gavana wa  Texas  Greg Abbott akiamuru bendera kupepea nusu mlingoti kutokana na janga hilo.

Rais Trump anatarajiwa kuzuru Texas siku ya Ijumaa akiambatana na mkewe Melania Trump 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii