Taarifa ya tume hiyo pia imeeleza watu waliojeruhiwa ni 107, wasiojulikana walipo ni 2, huku 532 wamekamatwa na Polisi wa nchi hiyo, na thamani ya uharibifu wa mali bado haijuulikani.
Waziri wa usalama wa ndani Kenya awasifu polisi wa Nairobi kwa ‘kulinda maisha na mali’ huku watu 11wakiuawa katika maandamano
Marekani yachelewesha tozo ya juu lakini yatangaza viwango vipya kwa baadhi ya mataifa
Moja kwa moja
Idadi ya watu waliofariki kutokana na maandamano ya Sabasaba Kenya imefikia watu 31 kufikia jioni ya Jumanne, Julai 8, kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo, (KNCHR).
Taarifa ya tume hiyo pia imeeleza watu waliojeruhiwa ni 107, wasiojulikana walipo ni 2, huku 532 wakiwa wamekamatwa na Polisi, na thamani ya uharibifu wa mali bado haijuulikani.
Tume hiyo bado inafuatilia kwa karibu nchini kote na kufuatilia ripoti zote na matukio yanayohusiana na maandamano ya Sabasaba, ya tarehe 7 Julai, 2025.
Kwa upande mwingine, KNCHR imelaani ukiukaji wote wa Haki za Binadamu na kutaka uwajibikaji kwa wahusika wote, ikiwa ni pamoja na polisi, raia na wadau wengine wote.