Wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabab wanaendelea na mashambulizi yao katikati mwa Somalia Tangu mwanzoni mwa mwaka 2025, wamekuwa wakirejea kaskazini mwa Mogadishu, mji mkuu, eneo ambalo walikuwa wamefukuzwa Julai 13 mwaka huu waliteka mji wa Tardo katika Mkoa wa Hijran, jiji lililo njia panda.
Hii ni mbinu ya kimkakati kwa kundi la Al Shabab kuuteka mji huu Mji wa Tardo uko kwenye makutano ya barabara kuu kadhaa Kuudhibiti mji huu kunaweza kuwezesha harakati za kundi hili kwenda maeneo mengine katika jimbo hilo.
Mji wa Tardo uliwahi kuwa na ngome muhimu ya jeshi la Somalia Al Shabab wanadai kuwa hawakupata upinzani wowote Kulingana na chanzo cha kijeshi kilichonukuliwa na shirika la habari la Reuters, Al Shabab imewafukuza Macwiisely kutoka Tardo, wapiganaji wa ndani ambao walikuwawakipigana dhidi ya Al Shabab na kuwezesha mamlaka ya Mogadishu kurejesha udhibiti katika mwaka 2022 na 2023.
Kulingana na chanzo hiki, karibu askari mia kadhaa wametumwa kusaidia wapiganaji hawa wa ndani, na shambulio la kukabiliana linatayarishwa kujaribu kurejesha tena jiji chini ya himaya ya serikali.
Wiki iliyopita, Al Shabab waliteka mji jirani wa Muqokori, na kusababisha maelfu ya raia kukimbia. Mashambulizi ya kundi hilo yameongezeka maradufu tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Lengo lake linaonekana kuwa ni kuanzisha ukanda wa kijeshi na wa vifaa ili kuunganisha ngome zake za kihistoria.