Iran kutorudi kwenye meza ya mazungumzo

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema hakuna uwezekano wa nchi yake kurejea katika mazungumzo na Marekani kwa sasa, hadi pale itakapohakikishiwa usalama na kutoshambuliwa tena.

Akizungumza na kituo cha CBS Evening News cha Marekani, Araghchi alieleza kuwa pamoja na matamshi ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba mazungumzo ya nyuklia yanaweza kuanza tena mapema wiki hii, Iran bado inahitaji muda zaidi kabla ya kujihusisha tena katika mazungumzo hayo.

Kauli hiyo inakuja baada ya hali ya mzozo kati ya Iran, Israel na Marekani kuzidi kuwa tete, kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na Israel dhidi ya maeneo ya nyuklia ya Iran, huku Marekani ikishiriki kwa kulipua maeneo ya Fordo, Natanz na Isfahan mnamo Juni 21.

Mazungumzo kati ya Iran na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia yalivunjika kufuatia mashambulizi hayo, na sasa matarajio ya kurejea mezani yanaonekana kusuasua.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii