Finland imeorodheshwa ya kwanza kama nchi yenye watu wenye furaha zaidi duniani kwa mwaka wa nane mfululizo. Kulingana na ripoti ya Furaha ya Dunia iliyochapishwa leo Alhamisi Machi 20, 2025 siku ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya furaha nchi hiyo imekuwa kidedea. Nchi ya Finland au Ufini ina jumuiya tatu.
Wafini wenyewe ambao ni asilimia 90 ya wakazi wote nchini humo, Waswidi wenye asili ya Sweden wako hasa upande wa kusini mwa nchi, kwa jumla ni takriban asilimia 5 ya wakazi wote nchini humo; hasa visiwa vya Aland ambapo kuna Waswidi watupu.Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji; wako wachache, jumla yao haifikii asilimia 0.2 ya wakazi wote. Mbali na hao, kuna wahamiaji asilimia 5.9, hasa kutoka Russia, Estonia na Somalia. Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya Kati, haina uhusiano na lugha za Kihindi.
Upande wa dini, asilimia 72 ni Walutheri na asilimia 1.1 ni Waorthodoksi. Madhehebu hayo mawili ya Ukristo yanatambulika na kupewa nafasi katika matukio mbalimbali na shuleni. Asilimia 1,6 wanafuata dini au madhehebu mengine. Nchi ambayo ni ya mwisho kwa wananchi wake kutokuwa na furaha duniani ni Afghanistan.