Real Madrid wanataka kocha Xabi Alonso kuanza majukumu ya kuwa meneja wao mpya mapema ili kukiandaa kikosi hicho kujiandaa na michezo ya kombe la Dunia kwa vilabu litakaloanza mwezi ujao.
Vyanzo vya habari vinasema Alonso, 43, atasafiri hadi Madrid tarehe 1 Juni kuandaa timu kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa michuano ya kwanza ya Fifa mnamo Juni 18 dhidi ya Al-Hilal ya Saudia huko Miami.
Kiungo huyo wa zamani wa Real, Liverpool na Uhispania Alonso alitangaza Ijumaa kuwa ataondoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani mwishoni mwa msimu.
Kocha wa sasa wa Real Carlo Ancelotti ataondoka mwishoni mwa Msimu na anahusishwa kwenda kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil.
Bado Real bado haijathibitisha hadharani kuhusu kuondoka kwa Ancelotti au kuwasili kwa Alonso.