ACHENI WASANII WAISHI MAISHA YAO - OMAR HARDWICK

Nyota wa filamu ambae amejipatia umaarufu zaidi kupitia Tamthilia ya Power , Omari Hardwick ameungana na baadhi ya watu kuwatetea wasanii ambao walipata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za awali wakati wa kuapishwa kwa Raisi wa Marekani Donald Trump .

Mapema wiki iliyopita kuliibuka ukosoaji ambapo rapa Snoop Dogg, Nelly, Soulja Boy & Rick Ross walipokea ukosolewaji kutoka kwa mashabiki sambamba na watu wengine maarufu kutokana na kitendo chao cha kutumbuiza kwenye sherehe za awali katika uapisho wa Raisi Donald Trump na kukiiita kitendo hiko kama Usaliti.

Nyota huyo wa filamu Omari Hardwick ametoa pia mtizamo wake juu ya jambo hilo wakati akifanya mahojiano na TMZ ambapo, Omari Hardwick ameeleza kwamba, mashabiki wanapaswa kuwapa nafasi wasanii waweze kufata au kufanya mambo yao mengine binafsi na sio kuona kama wamesalitiwa kutokana tu na utofauti wa mitizamo ya kisiasa.

Omari ameongoza kuwa miongoni mwa vitu ama jambo zuri kuhusu Muziki wa Hip-Hop ni kwamba .. Ni aina ya Muziki ambayo inamruhusu msanii kueleza kile ambacho anajihisi kwa wakati huo bila ya kuyumbishwa.

Katikati ya wiki iliyopita mtangazaji Stephen A Smith yeye pia aliwatetea wasanii wote walio tumbuiza kwenye uapisho wa Raisi Donald Trump na kusema kwamba.

Hawapaswi kuonekana kama wasaliti kwa sababu wamepata pesa akimtolea mfano Soulja Boy... Lakini pia kwa upande wa Snoop Dogg anasema kwamba , Snoop amekua akisaidia watu wengi kwenye jamii na hawezi kuisaliti jamii yake watu wasichanganye siasa na maisha binafsi walikwenda kwa ajili ya kutumbuiza na hawakwenda pale kama watu ambao wana unga mkono chama fulani cha siasa.

Kutokana na swala hili mpaka hivi sasa Snoop Dogg amepoteza zaidi wa wafuasi Laki 5 kwenye mitandao ya kijamii ambapo ni kwa mtandao wa Instagram pekee na kwa upande wa Nelly mauzo ya nyimbo zake yameshuka kwa asilimia 5%.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii