Marekani kusitisha michango ya moja kwa moja kwenye majukwaa ya UN

Marekani imeweka bayana kwamba haitakuwa ikitoa mchango wa moja kwa moja kwa majukwaa ya Umoja wa Mataifa yakiwemo maendeleo endelevu pamoja na malengo mengine ya kimataifa ikijumuisha kutokomeza umaskini, katika upigaji kura kwenye  Baraza Kuu la Umoja huo Jumanne.

“Kwa hiyo Marekani inakataa na kupinga Agenda 2030 ya maendeleo endelevu na malengo ya maendeleo endelevu na haitayathibitisha tena kama jambo la kawaida,” mwakilishi wa Marekani Edward Heartney ameliambia Baraza hilo.

Marekani ilipiga kura dhidi ya azimio la Siku ya Kimataifa ya Kuishi Pamoja kwa Amani ambalo lilithibitisha tena Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, ikikiri kwamba hii inajumuisha nia ya dhati ya kuhamasisha amani na kukuza jamii zenye amani na umoja kwa maendeleo endelevu, kutoa fursa ya haki kwa wote na kujenga taasisi zenye ufanisi, zinazowajibika na shirikisho katika ngazi zote.

Heartney alisema kwamba Wamarekani walipiga kura kwenye uchaguzi wa Novemba ili kuangazia zaidi kwenye maslahi ya Marekani. “Kwa kifupi, masuala kama Agenda 2030 yalipotea kwenye sanduku la kura,” alisema Heartney. Mataifa 162 yalipiga kura ya kuunga mkono Agenda hiyo wakati matatu ambayo ni Marekani, Israel na Argentina yakipinga.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii