Mfahamu kiongozi wa ISIS asiyeonekana aliyeuawa na makomando wa Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza operesheni maalum ya kumuua kiongozi wa ISIS Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi.

"Wanajeshi wote waliohusika katika operesheni hiyo wamerudi salama aliongezea Joe Biden.

"Ahsante sana wanajeshi wote walio na ujuzi na majasiri , tumemuua Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi," taarifa ya Ikulu ya whitehouse ilisema.

Rais alisema kwamba hivi karibuni atalihutubia taifa kuhusu shambulio hilo.

Al-Qurayshi alikuwa na wadhfa wa naibu wa ISIL ambaye alimrithi Abu Bakr al-Baghdadi alipofariki kama mkuu wa kundi hilo .

Vyombo vyote vya kijasusi nchini Iraq na Marekani vimemtambua Abu Ibrahim al-Hashmi al- Qurayshi kuwa Abdullahi Qardaash au haji Abdullahi , kulingana na habari zilizofichuliwa kuhusu mtu huyo.

Wizara ya haki nchini Marekani ilikuwa imeahidi zawadi ya $ 10m kwa mtu yeyote ambaye angesaidia kupatikana kwa kiongozi huyo wa ISIS na maeneo alipo .

Hashmi al Qurayshi ni

Mji wa Mahlabiya, ambao wengi wa wakazi wake ni raia wa Uturuki ulio umbali wa kilomita 20 kutoka Mosul, ndipo alipozaliwa kiongozi mpya wa ISIS Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qureyshi.

Jina halisi la Al-Qardaasi ni mwanamfalme Muhammad Said al-Salbi al-Malwa, kulingana na vyanzo vya kijasusi.

Alizaliwa mwaka wa 1976 katika mji wa Mahlabiya Kaunti ya Ninenah. Ana wake wawili na watoto 7, mdogo wao ni Prince na watoto tisa wa kike.

Baba yake Al-Qurayshi alikuwa imamu katika msikiti wa Furqan huko Mosul kuanzia 1982-2001.

Kabla ya kugunduliwa mwaka 2010 kiongozi wa ISIS, al-Baghdadi, ambaye aliuawa na Marekani, alihusishwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja na al-Qurayshi, kulingana na nyaraka zilizopatikana.

Al-Qurayshi anaaminika kujiunga na ISIS mwaka 2003-2004, mtu anayeelezwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kijeshi na kijasusi na alikuwa mhusika mkuu katika operesheni za ISIS.

Idara ya kijasusi ya Iraq inaamini kuwa ISIS imemficha al-Qardaash dhidi ya vita ili kumzuia asidhuriwe kwani ISIS inamhesabu mtu huyo kama mrithi wa al-Baghdadi.

Qardash alipata mafunzo ya mahakama katika Chuo cha al-Imam al-Adami huko Mosul.

Mwanzoni mwa operesheni hiyo, gaidi huyo alilipua bomu na yeye na familia yake, wakiwemo watoto na wanawake, waliuawa," afisa mkuu wa Marekani aliambia Reuters.

Katibu wa waandishi wa habari wa Pentagon John Kiby alisema operesheni ya Alhamisi iliyomuua kiongozi wa ISIS ilikuwa "ushindi kamili" na ilionyesha mafanikio ya vita dhidi ya ugaidi.

Wafanyakazi wa dharura wa Syria wanasema watu 13, ikiwa ni pamoja na watoto sita na wanawake wanne, waliuawa katika mlipuko kabla ya operesheni.

Wakaazi wa eneo ambalo operesheni hiyo ilifanyika walisema waliona helikopta ikitua kwenye eneo la tukio na milio mikubwa ya risasi kutoka kwa pande zinazozozana ikasikika.

Al-Qureyshi alikuwa na walinzi waliokuwa na silaha nzito huku akipigana kwa saa kadhaa na wanajeshi wa Marekani waliouawa katika operesheni hiyo.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii