TikTok yataka isiuzwe Marekani

Mahakama ya Juu ya Marekani, Jumatano imeamua kusikiliza maombi ya TikTok na kampuni yake mama ya China, ByteDance, kuzuia sheria iliyokusudia kulazimisha uuzwaji wa TikTo ifikapo Januari 19 au kupigwa marufuku kwa misingi ya usalama wa taifa.

Majaji hawakuchukua hatua mara moja kwa maombi ya dharura ya TikTok na ByteDance, pamoja na baadhi ya watumiaji wake walioweka maudhui yenye lengo la kusitisha marufuku ijayo, badala yake waltasikiliza hoja zao Januari 10.

Wanaopinga wanakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya chini uliozingatia sheria hiyo. TikTok inatumiwa na Wamarekani wapatao milioni 170 mpaka sasa. Bunge la Marekani, lilipitisha shauri hilo mwezi Aprili na Rais Joe Biden, alitia saini kuwa sheria rasmi.

Wizara ya sheria ya Marekani ilisema kuwa kama kampuni ya China, na mtandao wake wa TikTok unaleta tishio la usalama wa taifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii