Watu 26 wamefariki dunia Jumatano baada radi kupiga katika waya inayobeba umeme mwingi katika vitongoji vya mji mkuu wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, na kuangukia nyumba na soko serekali imesema.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba watu 24 waliyofariki dunia walikuwa ni wanawake, na wanaume wawili huku wengine wawili walijeruhiwa vibaya kwa mujibu wa ujumbe wa Twitter wa msemaji wa serekali ya Congo Patrick Muyaya.
Nyaya za umeme mara kwa mara zimekuwa zikianguka jijini Kinshasa, mji wenye wakazi milioni 13,na ambao pia miundombinu yake imepitwa na wakati pamoja na kuwepo makazi ya watu yasiyo ramsi hasa kwenye maeneo ambako hakujatengwa kuwa makazi ya watu.
Chama cha wasanifu majengo cha Congo katika taarifa yake kuhusiana na ajali hiyo, kimesema vifo hivyo vingeepukika, na ni kutokana na tukio la kutoheshimu kanuni za mipango miji kwenye njia za umeme mkubwa.