Watu 25 wauwa na umeme sokoni Kinshasa

Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa watu wasiopungua 25 wamekufa katika mjini mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa, baada ya waya wenye kiwango cha juu cha nguvu ya umeme kukatika na kuanguka sokoni na kwenye nyumba za makaazi ya watu leo Jumatano. Mkuu wa polisi katika jiji la Kishasa Sylvano Kasongo amesema ajali hiyo imetokea katika wilaya ya Matadi-Kibala, na kwamba watu kadhaa walipoteza maisha hapo hapo. Picha za vidio kutoka katika soko lililokumbwa na mkasa huo zimeonyesha watu wakilia kwa uchungu, huku maiti za wenzao zikilala katika madimbwi ya maji walikoanguka, na bidhaa za shambani zikitapakaa karibu na maiti hizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii