Maporomoko ya udongo yaua 14 Ecuador

Watu wasiopungua 14 wamekufa na wengine 32 wamejeruhiwa na maporomoko ya udongo yaliyotokea usiku wa kuamkia kaskazini mwa mji mkuu wa Ecuador, Quito. Ofisi ya msaada wa dharura nchini Ecuador ndiyo imetoa taarifa hizo kupitia ukurasa wa Twitter wakati vikosi vya uokozi vinaendelea na juhudi za kuwatafuta watu kwenye nyumba na mitaa iliyofunikwa kwa tope.

Mvua kubwa iliyonyesha Jumatatu usiku ilipelekea kufurika kwa maji kwenye korongo moja lililo jirani na mitaa ya watu wa kipato cha chini kabla ya baadaye kusababisha maporomoko ya mawe na udongo kwenye eneo hilo.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha mafuriko ya maji ya tope yakikatiza mitaani huku watu wakipiga kelele kuomba msaada.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii